Skip to content Skip to left sidebar Skip to footer

MAKUENI YAADHIMISHA SIKU YA KISWAHILI DUNIANI

Serikali ya Kaunti ya Makueni kupitia Idara ya Biashara, Masoko, Viwanda, Utamaduni na Utalii ikiongozwa na Waziri Sonia Nzilani leo imeadhimisha siku ya lugha ya Kiswahili duniani katika shule ya upili ya mabanati ya Makueni.

Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani ilianza Julai 7, elfu mbili na ishirini na mbili. Maadhimisho haya yalianzishwa na shirika la UNESCO ili kutambua umuhimu wa Kiswahili, lugha inayozungumzwa na watu wengi zaidi barani Afrika. Siku hii inaadhimisha jukumu la lugha katika kukuza tofauti za kitamaduni, kukuza umoja, na kuwezesha mawasiliano katika bara la Afrika na kwingineko.

Daktari Sonia aliwahimiza wanafunzi kutilia mkazo lugha ya Kiswahili kwa masomo yao kwa sababu lugha hii ni tajika na imeweza kufanywa lugha rasmi katika Jumuia ya Afrika Mashariki na Kati na pia kuanzishwa katika mitaala katika nchi za Magharibi. Maadhimisho haya yalihusu michezo ya kuigiza, neno nenwa, hadithi za urafa, utangazaji na nyimbo za Utamaduni.

Kwa kuongezea, lengo kuu la idara ya Utamanduni, Muziki na Sanaa Makueni ni kujenga tamaduni zetu na kuhakikisha lugha ya Kiswahili inaleta hisia za stahiki na ubunifu katika shule zetu na kwingineko.

Baadhi ya waliokuwemo ni mwalimu mkuu Bi. Mary Akoth, mkurungezi wa Utalii Bi. Dianah Muli miongoni mwa maafisa na waalimu wengine. Kwengineko, Maadhimisho kama haya Afrika Mashariki yalifanyika katika Ngome ya Yesu (Fort Jesus) leo kufuatia usiku wa Kiswahili uliosherehekewa hapo jana.

KiswahiliKidumu